Posts

Ijue sababu ya vijana kufeli kwenye kilimo

    MWANZO       Kufeli ni hali ya kukata tamaa baada ya kushindwa, pale unaposhindwa na kuamua kutoendelea ndipo unakuwa umefeli. Mfano:- Nelson Mandela, japokuwa alinyanyaswa,kufungwa na makaburu lakini hakukata tamaa mwisho wa siku akawa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.         Sasa tunakuja kwenye kilimo hususan kwetu Tanzania. Vijana wengi tunataka ndani ya muda mfupi  tuwe mamilionea kupitia kilimo au shughuli zingine, tukianguka mara moja  tuna ki ditch kilimo na hizo shughuli zingine, hapo ndipo tunakuwa tushafeli.    KILIMO KINAHITAJI NINI 1) KUJITOA 2) MUDA 3) NGUVU 4) MARUDIO 4) MOYO WA DHATI     Hapa nitasisitiza, kwa nini moyo wa dhati?? Kwa sababu unavyolima hulimi kwa ajili yako, bali unalima kulisha watu, hivyo moyo wa dhati lazima uwe nao, ila kama unaingia kwenye kilimo as a part time job you wil never make it.     KILIMO NI BIASHARA   ...

Ongeza kipato kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Image
Utangulizi Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwenye nchi zinazoendelea hususan Tanzania na Afrika kwa ujumla umekuwa ni wa mazoea. Wafugaji wameshindwa kugeuza mradi huu kuwa biashara na kujiongezea kipato cha kaya zao. Hii imetokana na ukosefu wa elimu ya ufugaji, ukosefu wa mabanda bora, uwepo wa magonjwa mbalimbali kama mdondo na ndui, pia upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa. ufugaji kuku Matokeo yake yamekuwa ni upatikanaji haba wa mazao yatokanayo na kuku. Mambo ya kuzingatia katika banda. * Banda liwe na urefu wa kutosha kumuwezesha mfugaji kuingia ki urahisi na kufanya usafi. * Banda lijengwe mahali pasipotuamisha maji au madimbwi ya mbu. * Banda liwe na madirisha ya kutosha yanayopitisha mwanga na hewa * Weka pumba za mpunga au maranda bandani kiasi cha sentimeta 4-6 * Gawa vyumba katika banda lako ambapo kuwe na maeneo ya kutotolea vifaranga na chumba cha majike yanayotaka kuatamia. Aina za kuku wa kienyeji * Kuchi * Ching'wekwe(umbo dogo) * Singamagazi ( hupatikana Tab...

UTAJIRI AMBAO KIJANA ANAWEZA KUPATA KUTOKANA NA KILIMO CHA MATIKITI

Image
MWANZO Kilimo cha matikiti Matikiti ni zao la kitropiki ambalo huwapatia vijana wengi kazi za kufanya zao hili hulimwa kwa wingi mikoa kama Morogoro, Tanga, Pwani, Lindi na hata Dar es Salaam. Zao hili ni jamii ya maboga, matango na hata ma squash. UTAYARISHAJI WA SHAMBA Shamba linatakiwa liwe limelimwa vizuri kwa kutifuliwa udongo maradufu ili uwe laini kusaidia mbegu kuweza ku mea vizuri. UPANDAJI Mbegu 500gms zinahitajika kwa shamba la 1eka ambazo gharama yake ni 300000/=. Upandaji ni 20000/= na upigaji wa mashimo ni 20000/= hapo kumbuka kulima kwa trekta ni 50000/= DAWA NA HUDUMA Dawa zinazohitajika ni Dudu-accelametin, folliar na fungicides ambazo kwa eka mpaka mavuno ni 150000. Upigaji wa dawa ni mara moja kwa wiki PALIZI NA MBOLEA Palizi ni baada ya wiki tatu ambayo bei yake ni 40000/= mbolea inayotakiwa ni Yaramilla @ 40000/= na mbolea ya pili ni Yaramilla nitrabor @ 40000/= hii tunaweka pale matunda yanapoanza kwaajili ya kuongeza s...

Fulsa ya kufanya kazi ya uandishi wa makala kwenye blog

Tunatumaini u mzima wa afya, Tunamshukuru Mungu kwa hilo, Mpenzi mfuatiliaji wa makala za ufugaji na kilimo kwenye app ya ufugaji tunapenda kutangaza fulsa ya uandishi wa makala za kuelimisha jamii kwenye blog. Kwa sasa tunahitaji waandishi wa makala za ufugaji, Kilimo, Ujasiriamali, makala za ushauri wa mahusiano ya kimapenzi, ndoa, na makala za kuhamasisha wanafunzi kujisomea kwa bidii na kuwapa mada za kimasomo, Makala za kufundisha watu kufanya usaili au interview kwa ufasaha na kutoa taarifa za nafasi za kazi kwenye blog husika. Malipo: unalipwa kwa idadi ya wanaosoma blog unayoandika, Mfano blog ikisomwa na watu elfu 50 unalipwa laki moja. Kama unauwezo wa kuandika makala kati ya hizo zilizotajwa hapo juu basi andika makala moja ya mfano ambayo haijawekwa kwenye mtandao wowote duniani kisha itume kwenda mkuublog@gmail.com kumbuka kuweka namba zako za simu na email mwisho wa makala ili tuweze kuwasiliana nawe kama tutaona unafaa.

Karibu sana kwenye app ya ufugaji app ya kwanza nchini Tanzania

Image
Hallooo msomaji wa app ya ufugaji unakaribishwa sana kwenye app hii ya ufugaji ambayo ni app ya kwanza Tanzania kukuletea makala zote za ufugaji wa kuku, bata, kanga, na mifugo mingine. App hii haijaishia kukufundisha ufugaji tu bali unapata mafunzo ya kulimo biashara. Hapa utajifunza jinsi ya kulima mazao ya aina zote kibiashara na tunakuja na mpango wa kukupa habari za kilimo kama kukutafutia masoko ya bidhaa zako. Hakuna app ya ufugaji kama hii. Asikudanganye mtu. Kaa na app hii kwenye simu yako kisha wewe mwenyewe utajua mbivu na mbichi. Tumedhamiria kumuunga mkono Mh Rais wetu wa awamu ya Tano J.P.Magufuli katika kuitengeneza Tanzania ya Viwanda. Bila kuipigia upatu sekta ya kilimo viwanda vyetu havitapata malighali za kutosha. App hii inakuja na mpango kabambe ambao utakunufaisha wewe pia msomaji zaidi ya kupata pafunzo ya kilimo na mifugo. Tutakuwa tunatoa zawadi za vocha za simu mara kwa mara ndani ya app ya ufugaji. Hivyo ukiziwahi vocha hizo kabla ya wenzio basi ni z...