Ongeza kipato kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji
Utangulizi Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwenye nchi zinazoendelea hususan Tanzania na Afrika kwa ujumla umekuwa ni wa mazoea. Wafugaji wameshindwa kugeuza mradi huu kuwa biashara na kujiongezea kipato cha kaya zao. Hii imetokana na ukosefu wa elimu ya ufugaji, ukosefu wa mabanda bora, uwepo wa magonjwa mbalimbali kama mdondo na ndui, pia upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa. ufugaji kuku Matokeo yake yamekuwa ni upatikanaji haba wa mazao yatokanayo na kuku. Mambo ya kuzingatia katika banda. * Banda liwe na urefu wa kutosha kumuwezesha mfugaji kuingia ki urahisi na kufanya usafi. * Banda lijengwe mahali pasipotuamisha maji au madimbwi ya mbu. * Banda liwe na madirisha ya kutosha yanayopitisha mwanga na hewa * Weka pumba za mpunga au maranda bandani kiasi cha sentimeta 4-6 * Gawa vyumba katika banda lako ambapo kuwe na maeneo ya kutotolea vifaranga na chumba cha majike yanayotaka kuatamia. Aina za kuku wa kienyeji * Kuchi * Ching'wekwe(umbo dogo) * Singamagazi ( hupatikana Tab...