Ongeza kipato kupitia ufugaji wa kuku wa kienyeji

Utangulizi

Ufugaji wa kuku wa kienyeji kwenye nchi zinazoendelea hususan Tanzania na Afrika kwa ujumla umekuwa ni wa mazoea. Wafugaji wameshindwa kugeuza mradi huu kuwa biashara na kujiongezea kipato cha kaya zao. Hii imetokana na ukosefu wa elimu ya ufugaji, ukosefu wa mabanda bora, uwepo wa magonjwa mbalimbali kama mdondo na ndui, pia upatikanaji haba wa chanjo za magonjwa.
ufugaji kuku


Matokeo yake yamekuwa ni upatikanaji haba wa mazao yatokanayo na kuku.

Mambo ya kuzingatia katika banda.


* Banda liwe na urefu wa kutosha kumuwezesha mfugaji kuingia ki urahisi na kufanya usafi.


* Banda lijengwe mahali pasipotuamisha maji au madimbwi ya mbu.


* Banda liwe na madirisha ya kutosha yanayopitisha mwanga na hewa


* Weka pumba za mpunga au maranda bandani kiasi cha sentimeta 4-6


* Gawa vyumba katika banda lako ambapo kuwe na maeneo ya kutotolea vifaranga na chumba cha majike yanayotaka kuatamia.

Aina za kuku wa kienyeji
* Kuchi

* Ching'wekwe(umbo dogo)

* Singamagazi ( hupatikana Tabora)

* Mbeya

* Pemba

* Unguja

* Kishingo


Magonjwa ya kuku


Newcastle(kideli)

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Dalili zake ni kuharisha choo cha kijani na njano, kukohoa na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula , kutoa kamasi na machozi


Kinga ya ugonjwa huu ni newcastle vaccine kwa utaratibu wa siku 3, wiki 3 na miezi 3.


Minyoo

Minyoo kama chango na tegu huathiri kuku wa kienyeji. Kuku hukosa hamu ya kula na mayai hupungua. Mchanganyiko wa dawa tatu hutumika kuangamiza minyoo, dawa hizi ni nipiperazine,phenothiazine, na butynorate. Dawa hizi ziko katika mfumo wa vidonge, tumia kidonge 1 kwa kuku mzima na nusu kwa vifaranga.

Magonjwa ya mapafu

Magonjwa haya huathiri mfumo wa hewa na kuambatana na mate na sauti kama kikohozi. Dalili zake ni vidonda vyenye utando wa kahawia usoni na chini ya midomo, kukosa hamu ya kula na vifo vingi.

Kinga yake ni kuchanja vifaranga vikiwa na umri wa mwezi 1-2 kwa kutumia chanjo ya fowl pox vaccine

Ni muhimu mfugaji akawapa kuku wake vitamin A, kwani upungufu wa vitamin A huathiri zaidi kuku wadogo na wanaokua na mara nyingi hupelekea vifo

Faida za ufugaji kuku wa kienyeji

* Hutupatia fedha kwa kuuza nyama na mayai


* Mayai yana madini muhimu kama methionine na cystine ambayo ni muhimu kwa watoto wachanga

* Kinyesi cha kuku ni mbolea kwa matumizi ya shambani


* Kiwanda asili cha kutotolesha vifaranga badala ya incubators ambazo ni gharama kubwa


* Manyoya ya kuku hutumika kutengeneza mapambo mbalimbali, mito na magodoro

Hitimisho

Kuku ndiye mnyama pekee anayeweza kufugwa mahali popote hapa ulimwenguni. Na ufugaji wa kuku ndiyo shughuli inayofanyika kwa wingi duniani kuliko ufugaji mwingine wowote ule. Ewe mjasiriamali kumbuka wingi wa mifugo yako ndio wingi wa kipato chako hivyo kumbuka kanuni hii "start small dream big


By Dennis Kavana


Cell:-0687568630
Imehaririwa na App ya Kilimo

Comments

Popular posts from this blog

Ijue sababu ya vijana kufeli kwenye kilimo

Fulsa ya kufanya kazi ya uandishi wa makala kwenye blog