Ijue sababu ya vijana kufeli kwenye kilimo
MWANZO
TANGAZO bado tunahitaji vijana wa kufanya kazi ya uandishi wa makala za kilimo na ufugaji tuma mfano wa makala ambayo umeiandika mwenyewe kwenda mkuublog@gmail.com
Kufeli ni hali ya kukata tamaa baada ya kushindwa, pale unaposhindwa na kuamua kutoendelea ndipo unakuwa umefeli. Mfano:- Nelson Mandela, japokuwa alinyanyaswa,kufungwa na makaburu lakini hakukata tamaa mwisho wa siku akawa Rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini.
Sasa tunakuja kwenye kilimo hususan kwetu Tanzania. Vijana wengi tunataka ndani ya muda mfupi tuwe mamilionea kupitia kilimo au shughuli zingine, tukianguka mara moja tuna ki ditch kilimo na hizo shughuli zingine, hapo ndipo tunakuwa tushafeli.
KILIMO KINAHITAJI NINI
1) KUJITOA
2) MUDA
3) NGUVU
4) MARUDIO
4) MOYO WA DHATI
Hapa nitasisitiza, kwa nini moyo wa dhati?? Kwa sababu unavyolima hulimi kwa ajili yako, bali unalima kulisha watu, hivyo moyo wa dhati lazima uwe nao, ila kama unaingia kwenye kilimo as a part time job you wil never make it.
KILIMO NI BIASHARA
Vijana tunasahau kwamba tunalima ili tuuze, ukishalitambua hilo basi, mawazo yako yatakuwa ni ya kijasiriamali. Lakini vijijini na hata mijini wengi tumekuwa tukilima kwa mazoea. Marekani asilimia chini ya 5 ni wakulima na wanazalisha kwa ajili ya nchi nzima. Lakini Tanzania asilimia zaidi ya 60 ni wakulima lakini hatujitoshelezi.
NINI TUFANYE
1)TUSILIME KWA MAZOEA
2)TUTUMIE UMWAGILIAJI
3)TUWATUMIE WATAALAMU
4)TUTUMIE MBEGU BORA
5) TULIME KIJASIRIAMALI
HATAMU
Mafanikio huja kwa kufanya sio kujaribu. Hivyo ndugu zangu wakulima wapya na watarajiwa, siku huisha baada ya masaa 24, hivyo usitegemee kilimo kikakulipa ndani ya masaa 48. Kuwa na malengo, ukianguka simama kaza then utaona reward ya kilimo
TANGAZO bado tunahitaji vijana wa kufanya kazi ya uandishi wa makala za kilimo na ufugaji tuma mfano wa makala ambayo umeiandika mwenyewe kwenda mkuublog@gmail.com
Comments
Post a Comment